Sunday, April 10, 2011

GADDAFI KUITIKIA WITO WA AU KUSITISHA MAPIGANO.....

Rais wa Akrika ya Kusini Jacob Zuma akifatana na viongozi wengine watatu wa Afrika walikutana na kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi mjini Tripoli kwajili ya mazungumzo ya Amani ya kuinusuru nchi hiyo ya libya wakati wa mazungumzo hayo kiongozi wa libya kanali gaddafi alikubali kuwepo na mazungumzo ya pamoja ya kuleta amani nchini libya Zuma alisema ni vyema kusitisha mapigano mara moja ili kuweza kufungua milango ya misaada kwa nchi hiyo, na kwa upande wa kiongozi wa upinzani wa waasi Guma Al-Gamaty amesema kuwa wataangalia kwa makini mpango huo wa Umoja Wa Afrika lakini alisisitiza kuwa hawatokubaliana na mpango wowote wa kumuacha Kanali Gaddafi au watoto wake kuongoza nchi hiyo ya Libya.

No comments:

Post a Comment