Yule mwana nchi aliechomwa moto kwa kosa la kuzamia Disco afariki dunia wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu Lilah alifariki jana jioni na mipango ya mazishi inafanya huko kigamboni ambapo inategemewa kuzikwa leo jioni katika makaburi ya mji mwema. marehemu Lilah ambaye alikuwa mfanya biashara maarufu wa nguo za kuogelea na vitu vya kitamaduni kwa waendao beach za kigamboni alikumbwa na mauti baada ya kukutwa ndani ya Disco akiwa hana tiketi maalumu inayovaliwa mkononi kwa wale wote wanaoingia ndani ya ukumbi huo wa south beach.
Spoti na starehe ni mmoja wa marafiki wa marehemu kwani alikuwa akitembelea na kuuza bidhaa zake katika ufukwe mbali mbali za kigamboni ikiwemo chadibwa beach. marehemu Lilah alikamatwa na walinzi wa fukwe ya south beach jumapili iliyopita kwa kudaiwa kuingia bila kulipa kiingilio cha Disco linalopigwa kila mwisho wa wiki ufukweni hapo, Lilah baada ya kushikwa hatimaye alipelekwa mwa meneja wa hotel hiyo ambaye aliamrisha achomwe moto
Akiongea kwa taabu na muandishi wetu katika Hospital ya kigamboni kabla ya kuhamishiwa muhimbili alikoagia dunia, marehemu Lilah alisema hata kupona pale alimshukuru mungu maana kwa kipigo na moto ule. (habari zaidi na Spoti Starehe blog)
No comments:
Post a Comment