
Waziri Mkuu wa Japan Naoto Kan hii amesema kuwa viwango vya miale ya sumu vimezidi katika kinu cha nyulia kilicho athirika na tetemeko la ardhi, baada ya kutokea mlipuko mwingine hii leo na kuwa kuna hatari ya sumu hiyo kuvuja na kuingia hewani.
Kan amewaomba watu walio umbali wa kilomita 30 kutoka kinu hicho kilipo Kaskazini mwa mji mkuu wa Tokyo wajifungie ndani.
Mlipuko wa hii leo ni wa tatu katika kinu hicho tangu kuathiriwa na tetemeko la ardhi na tsunami siku ya Ijumaa iliyopita, ambapo maafisa wa serikali wamekuwa wakijaribu kuzuia kuyeyuka kwa mafuta kwenye vinu hivyo vitatu vya Fukushima Daiichi kwa kuvimwagia maji ya baharini ili kuvipooza.
Huku kukiwa na wasiwasi kuhusu athari ya kuanguka uchumi kutokana na majanga hayo mawili, hisa za Japan zimeshuka kwa asilimia 7.0, hadi viwango vyake vya chini ambavyo havijafikiwa kwa kipindi cha miaka miwili.
No comments:
Post a Comment