Tuesday, March 22, 2011

BREAKING NEWS.....KUNDI LA FIVE STARS TAARAB LIMEPATA AJALI

Ajali mbaya na yakusikitisha imetokea usiku wa kuamkia leo huko mikumi mkoa wa morogoro na kusababisha vifo vya watu 13 na wengine 9 kujeruhiwa vibaya ajali hiyo ambayo basi dogo lililobeba kikundi cha taarabu cha five stars liligongana na lori lililokuwa limesheheni mbao.

Mpaka sasa majina ya wanamuziki wa bendi hiyo ya five stars modern taarab waliopoteza maisha ni kama ifuatavyo Nassor madenge Issa kijoti Fembe juma Omary hashim Tizo omari Ngeleza Hassan Hamisa omari Maimuna Mapande Haji msaniwa 

Kwa upande wa majeruhi wa ajali hiyo ni kama ifuatavyo Mwanahawa Ally (55) ambae alikuwa ni mualikwa katika safari hiyo akitokea katika bendi ya East African Melody, Susana Benedict (32) Samila Rajab (22) Ally Juma (25) Mwanahawa Hamisi (36) Rajab Kondo (25) Zena Mohamed (27) Shaban Hamisi (41) Msafiri Mussa (22) ambao wamelazwa katika hospital ya mkoa wa morogoro.

Bongonl inatoa pole kwa wale wote wahusika wa karibu wa marehemu na inawatakia matibabu mema majeruhi wote waliopo hospitali  ameen.

No comments:

Post a Comment